Pages

Sunday, December 9, 2012

TIMU YA GYMKHANA BINGWA WA BONANZA LA UHURU DAR CORPORATE BONANZA

KIKOSI CHA NMB

TASWA FC


Mbozi Katala wa TASWA FC  na Pastory wa NMB wakipambana kwenye mchezo wa awali, hata hivyo walitoka sare ya 1-1


Azam Group

Gymkhana FC
Bonanza la kusheherekea miaka 51 ya uhuru wa Tanganyika linaloendelea kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam leo limeanza kuto mwelekeo wa timu zitakazoingia robo fainali.

Bonanza hili limedhaminiwa na  kampuni ya Vennedrick (T) Limited kupitia Mkurugenzi wake Fredrick Mwakalebela na kudhaminiwa na NMB banki.

Bonanza hili linaendeshwa kwa mtindo wa ligi na timu mbili toka kila kundi zitafuzu hatua ya nusu fainali na

Timu za Barrick, NMB, DSTV na Radio Times zipo kundi A na TASWA FC, Jubilee, Azam Group na wenyeji Gymkhana wapo kundi B

Mchezo wa awali Gymkana waliifunga Azam bao 1-0 na katika mchezo wa pili Gymkhana wakaifunga Barrick  mabao 3-1

NMB walitoshana nguvu na TASWA FC baada ya sare ya 1-1 na NMB wametoka suluhu na Times FM ya 0-0.

Michezo mingine Times wameifunga Jubilee bao 1-0, Azam walifungwa n Dstv bao 2-1, Jubilee wakifunga TASWA bao 1-0,

Kwenye michezo ya nusu fainali timu zilionyeshana umamba wa kupigana badala ya soka la uwanjani kwani TASWA walitolewa na waandaaji baada kutokea fujo wakati wa mchezo wao na Gymkhana, Gymkhana walikuwa wanaongoza kwa bao 1-0
Mchezo mwingine wa nusu fainali nao haukumalizika kwa NMB waliondoa timu uwanjani wakati Dstv wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0

Fainali nayo pia hakumalizika kwani Dstv walifanya fujo na mchezaji wao alipoonyeshwa kadi nyekundu waligoma kuendelea na kutoa timu uwanjani.

Waandaji wakatangaza Gymkhana kuwa mabingwa na timu yenye nidhamu wakiwa ni times Fm na kukabidhiwa kikombe kila mmoja

No comments:

Post a Comment