Pages

Saturday, December 8, 2012

TAIFA QUEENS BINGWA IFNA BILA KUFUNGWA , ANNA BAYI APEWA TUZO

TIMU ya taifa ya netiboli, Taifa Queens imetwaa ubingwa wa michuano ya kimataifa ya mchezo huo yaliyomalizika nchini Singapore bila kufungwa.

Taifa Queens imecheza na  Namibia na kuibugiza bila huruma na kuchukua kombe na medali za dhahbu huku mwenyekti wa CHANETA akipewa tuzo kwa kuwa kiongozi pekee aliyehudhuria fainali hizo kwa miaka minne mfulilizo.

Katika mchezo mingine, Taifa Queens ilicheza dhidi ya wenyeji Singapore na kuibuka na ushindi wa mabao 51-34.

Mashindano hayo yamefungwa jana

Michuano hiyo imeandaliwa na Chama cha Netiboli cha Singapore na kusimamiwa na Shirikisho la Kimataifa la Netiboli (IFNA)

No comments:

Post a Comment