Pages

Saturday, December 8, 2012

NI PROFESSIONAL NA TAYFA FAINALI YA LIGI YA U-17 MKOA WA DAR ES SALAAM

TIMU ya Professional ya Temeke leo imeifunga Makumbusho Talent ya Kinondoni kwa penalti 4-2 baada ya muda wa mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1  kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa leo asubuhi kwenye uwwanja wa Karume

Timu zote zilionyesha mchezo wa kuvutia na ufundi hali iliyovuta mashabiki kwani mashindano hayana kiingilio.

Professional ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 20 kupitia kwa Brian Hiza na Makumbusho wakasawazisha dakika ya 46 kupitia kwa mshambuliaji wao mahiri Ibrahim Kabwela.

Penalti za  Professional zimepigwa na Juma Hamisi, Shomari Pius, Ramadhan Mohamed na Shaban Seleman.
Makumbusho penalti zao zilipigwa na Simioni Kiliani na Kasim Juma. Waliokosa penalti kwa upande wa Makumbusho ni Shabaan Mtambo na Thabit Mshamu.

Nusu fainali ya Pili ilizikutanisha Majohe na TAYFA ambapo mpaka muda wa mchezo unamalizika Majohe na TAYFA wakiwa sare ya mabao 3-3.

Mabao mawili ya Majohe yalifungwa Mwinshehe Diwinge dakika ya 7 na dakika 28 na bao la tatu lilitiwa kimiani na Said Hassan dakika ya 10.

TAYSA yenyewe mabao yake yaliwekwa kimiani na James Michael dakika ya 13, Ramadhan Shaban dakika 20 na karamu ya mabao iliihitimishwa na Hassana Mazongera dakika ya 23.

Kutokana na kwamba mshindi lazima apatikane ilibidi wapigiane penalti kulingana na kanuni za ligi yenyewe na TAYSA wakafunga penalti 3 dhidi ya penalti 1 waliyoambulia Majohe.

Penelti za TAYSA zilifungwa na Ahmad Athuman, Ramadhan Shabaan na Said Hassan huku ile ya Majohe ilifungwa na Pius Lisoka.

Waliokosa penalti kwa Majohe ni Said Hassan, Faraja Said na Christopher Sospeter
Kikosi cha TAYFA

Golikipa wa Professional akiwa amebebwa kwa furaha ya ushindi baada ya kungaua penalti mbili

Mchezaji wa Professional akikimbia na mpira

Mashabiki wa Professional wakishangilia kuingia fainali



Kikosi cha Majohe


No comments:

Post a Comment