NYOTA wa Yanga Haruna
Niyonzima na Khamis Kiiza wanatarajiwa kuwasili nchini mwishoni mwa wiki hii
ili kujiunga na wenzao katika mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye uwanja
wa Bora Kijitonyama.
Akizungumza leo
uwanjani hapo Kocha Msaidizi wa timu hiyo fredy Minziro alisema kuwa wachezaji
hao walitarajiwa kuwasiri nchini tangu Jumapili iliyopita lakini badala yake
wataingi nchini wiki hii.
Kwa upande wake kiungo wa
Kimataifa wa Yanga, Niyonzima alipewa mapumziko ya wiki moja kwenda nchini kwao
Rwanda baada ya kurejea kutoka katika mashindano ya chalenji yaliyomalizika
mapema mwezi huu Kampala Uganda.
Wakati huo huo, Kocha huyo
alisema kuwa mazoezi ya timu yake yanampa morali ya kuona kwamba watakuja
kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Alisema kuwa wachezaji wake
wamekuwa wakifanya vizuri katika mazoezi jambo ambalo limekuwa likimpa hali ya
kuashiria mafanikio katika mechi za mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Minziro alisema kuwa ana
amini kuwa timu hiyo itafanya mabadiliko zaidi katika mzunguko wa pili wa ligi
hiyo kutokana na hali wanayoionesha wachezaji hao wakiwa mazoezini.
“Kadri siku zinavyozidi
kusogea mbele kuelekea mzunguko wa pili wa ligi wachezaji wangu wamekuwa
wakionesha kiwanga kizuri jambo ambalo limekuwa likinipa hali ya kuwa timu
itafanya makubwa zaidi kwenye mzunguko wa pili,” alisema Minziro.
No comments:
Post a Comment