Pages

Sunday, December 2, 2012

KILIMANJARO STARS USIPIME CECAFA



Timu ya taifa ya Tanzania Bara The Kilimanjaro Stars imefanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya michuano mataifa ukanda wa Afrika mashariki na kati maarufu kama michuano ya Chalenji kwa ushindi wa karamu baada ya kuichapa Somalia kwa mabao 7-0.

Mchezo huo kwa timu zote mbili ulikuwa ni mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi wakiwa katika kundo la B mchezo uliochezwa katika viwanja vya KCCA  ulioko Lugogo.

Mrisho Ngassa  alikandamiza goli 5 huku John John Raphael Bocco akifunga magoli mawili.

Ngasa alianza kuandika bao la kwanza dakika ya kwanza ya mchezo na kuanza kuamsha furaha za mashabiki kabla ya kuandika bao la pili  dakika ya 24 na baadaye John Bocco kuandika bao la tatu dakika ya 27 na lingine dakika ya 42.

Dakika moja kabla ya mchezo huo kwenda mapumziko Ngasa tena akaandika bao la tano na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu ndani ya mchezo mmoja ‘hat trick’ katika michuano ya mwaka huu.

Baada ya mapumziko wasomali walijaribu kuzuia lakini juhudi zao hazikua dafu pale Ngassa alipoandika bao la nne na la tano kwa Kilimanjaro katika dakika za 73 na 75.

Huo ndio ushindi mkubwa tangu michuano hiyo kuanza.
Mabao hayo matano ya Ngasa yanamfanya kuwa ndiye mfungaji anayeongoza mpaka sasa kwa kufunga magoli mengi huku John Bocco akimfuatia akiwa na magoli manne. 

Wakati Burundi wakikamilisha kwa ushindi wa bao 1-0 idi ya Sudan, Kilimajaro stars sasa itakuwa imemaliza hatua ya makundi ikishika nafasi ya pili na sasa ikitarajiwa kukutana na Rwanda katika hatua ya robo fainali.

Katika michezo ya kundi la C Malawi imefanikiwa kuifunga Zanzibar kwa mabao 2-0 mchezo uliochezwa katika uwanja wa Wankulukuku.

Mabao ya Malawi yamefungwa na Ndaziona Chatsalia na  Chiukepo Msowoya yakifungwa katika dakika za mapema.
Malawi imemaliza ikiwa katika nafasi ya pili katika kundi hilo ambalo limeongozwa na Rwanda baada yah ii leo kuichapa Eritrea kwa mabao 2-0.

Kwa upande wao Burundi wao wamewachapa Sudan kwa bao 1-0 mchezo uliofanyika katika uwanja wa at Wankuluku. Bao la washindi lilifungwa Chris Nduwagira kunako dakika ya 16 na hivyo Burundi wakimaliza hatua ya makundi bila ya kufungwa

No comments:

Post a Comment