Pages

Sunday, December 2, 2012

AZAM HAO KINSHASA KUTEST MAJEMBE MAPYA NA KOMBE LA JAMII

BEKI kisiki wa Tanzania Prisons David John Mwantika amesajiliwa na Azam FC na kufanya idadi ya mabeki waliosajiliwa na timu hiyo kuwa watatu.


Mabeki wengine waliosajiliwa ni Malika Ndeule na Omary Mtaki na Uhuru Selemani na kufanya jumla ya wachezaji waliosajiliwa na Azam FC kufikia wachezaji wanne.

Akizungumza jijini, Afisa Habari Jaffa Idd Maganga alisema kuwa wamesajili wachezaji hao ilikukipa nguvu kikosi chake katika mzunguko wa pili na kujaza nafasi za wachezaji waliosimamishwa.

"Tumesajili wachezaji ilikukiongezea makali kikosi chetu na kujaza nafasi za wachezaji waliosimamishwa wakati wa mzunguko wa kwanza", alisema Jaffa Idd.

Pia alisema kuwa Azam FC inatarajia kuelekea Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Disemba 13 hadi 23  kushiriki mashindano ya Ngao ya Jamii

Mashindano hayo yatashirikisha timu kubwa za kutoka Kongo kama DCMP na AS Vita Club timu kutoka nje ya Congo ni Azam FC, Tusker FC, Gombe United ya Nigeria na Diable Noirs na Congo Brazavile.

Azam FC itayatumia mashindano hayo kama maanadalizi ya kombe la Shirikisho. (Confederations Cup)

"Azam FC inahitaji maandalizi na mechi nyingi za kirafiki nje ya Tanzania ili kupata uzoefu kabla ya kushiriki kombe la shirikisho hivyo ni nafasi muhimu kwetu", alisema Jaffa Idd.

No comments:

Post a Comment