WAKATI
ligi kuu ya soka Zanzibar ikiwa katika mapumziko hadi baada ya
kumalizika sherehe za Mapinduzi mwezi ujao, timu mbalimbali za ligi hiyo
zimekuwa katika harakati za kuimarisha vikosi vyao.
Katika
mchakato huo, timu ya Chipukizi imeamua kuwatema wachezaji wake wanane
na kuwapeleka timu mbalimbali na kusajili wachezaji watatu wapya ili
kukiongezea nguvu kichosi hicho kilichopania kutwaa ubingwa wa Zanzibar
msimu huu.
Naibu Katibu Mkuu wa timu hiyo Adam AbadÃa, amesema kuwa wachezaji hao wapya wamesajiliwa kuongeza nguvu katika nafasi ambazo zilikuwa na kasoro wakati wa hatua ya kwanza ya ligi kuu.
Hata
hivyo, Katibu huyo hakuwa tayari kuyaweka hadharani majina ya wachezaji
hao wapya zaidi ya kusema ni wa nafasi ya kiungo wachezaji wawili na
mshambuliaji nafasi moja.
Chipukizi inatarajiwa kuweka kambi Mkoani Tanga hivi karibuni, ili kujiweka sawa kabla kwanza kwa ngwe ya pili ya ligi kuu.
Aliwataja
wachezaji wanane waliotemwa na timu yake kuwa ni Vuai Abdalla
aliyepelekwa Hard Rock na Ameir Daudi kwenda timu ya Machomanne, wote
kwa mkopo.
Katibu
Mkuu huyo ametoa wito kwa wachezaji wa timu hiyo kuripoti mapema
kujiandaa na kambi inayotarajiwa kuanza Disemba 20, mwaka huu mkoani
Tanga.
No comments:
Post a Comment