Pages

Tuesday, December 18, 2012

BERKO AFUZU

Berko afuzu majiribio FC Lupopo
Aliyekuwa kipa namba moja wa timu ya Yanga Yaw Berko amefanikiwa kusajiliwa katika timu ya FC Lupopo ya Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo.
Berko ambaye alitaka kuachwa na klabu yake aliondoka nchini hivi karibuni kwenda kwenye majaribio na hatimaye amefanikiwa kujiunga na klabu hiyo ambapo tayari klabu yake iliweka wazi kuwa asipofuzu majaribio hayo angetolewa kwa mkopo ili nafasi yake izibwe na pacha wa Mbuyu, Kabange Twite.

Katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema kuwa kuondoka kwa beko haitaifanya timu hiyo kuyumba  na wala haitafanya vibaya  katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
Alisema Yanga ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wenye uwezo mkuwa hivyo ni matumaini yake kuwa Ally Mstafa ‘Barthez’ pamoja na Said Mohamed wataziba vilivyo nafasi hiyo ya Berko.

“Ukiangalia hata katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu, Berko hakucheza mechi nyingi lakini timu ilifanya vizuri hivyo kuondoka kwake  hakutotufanya tuharibu kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu.
“Tunaimani kubwa na makipa wetu waliyopo hivi sasa  kuwa wana uwezo wa kuiongoza timu yetu kuhakikisha inafanya vizuri mzunguko wa pili kama ilivyo kuwa kwa ule wa kwanza kwa sababu wa uwezo na uzoefu na wamecheza ligi yetu kwa muda mrefu,” alisema Mwalusako.

Berko alijiunga na Yanga SC mwaka 2009, akitokea Liberty Proffessional ya Ghana baada ya uwezo wake wa kulinda lango kumvutia aliyekuwa kocha mkuu wa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mara 22 Kostadin Papic.
Katika hatua nyingine klabu hiyo leo inatarajia kuweka wazi wachezaji wake iliyowaacha na wale iliyowaongeza kwa kwa ajili ya kuhakikisha inatimza Lengo lake la  kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu  msimu huu ambao kwa sasa unashikiliwa na Simba.

No comments:

Post a Comment