Pages

Thursday, December 20, 2012

AKINA KABALA NA SUNZU KUTUA KESHO KUUNGANA NA WENZAO KUIKABILI TAIFA STARS

NYOTA wawili wa timu ya Taifa ya Zambia "Chipolopolo wanatarajiwa kuingia nchini kesho pamoja na Kocha Mkuu, Herve Renard.

Wachezaji hao Reinford Kalaba na Stopilla Sunzu ambao walikuwa kwenye tuzo za mwanasoka wa Afrika zilizofanyika nchini Ghana.

Akizungumza na wandishi wa habari, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema kuwa wachezaji hao pamoja na kocha watawasili leo kuungana na wenzao.

Wachezaji wengine wa timu ya Zambia waliwasili nchini juzi na jana wamefanya mazoezi kwenye uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Hata hivyo, benchi la ufundi la timu hiyo limeukataa uwanja wa Karume na kusema wao wanataka kufanya mazoezi kwenye uwanja wa nyasi za asili.

Mchezo wa Zambia na Taifa stars utachezwa kesho kutwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment