Pages

Saturday, November 17, 2012

SERENGETI BOYS KWENYE CHAKULA CHA JIONI HOTEL YA JB BELMONT












Kocha wa serengeti boys na kocha wa Congo brazaville wakiwa kwenye press

Timu ya taifa ya vijana Serengeti Boys jana usiku ilifanyiwa hafla fupi ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na kamati maalumu ya kuhamasisha watanzania kuichangia timu hiyo pamoja kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika mchezo wake dhidi ya timu ya vijana kutoka Congo Brazzaville ilifanyika katika hoteli ya JB Belmonte iliyo jijini,  Dar es Salaam.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali kwa lengo la kubadilishana mawazo, pamoja na kutunisha mfuko wa Serengeti ambao inahitaji shilingi milioni 162 ili kufanikisha azma ya kutinga fainali za mataifa ya Afrika, fainali ambazo zitafanyika mwakani nchini Morroco.

Rais wa shirikisho la soka nchini Leodgar Tenga alipata nafasi ya kusema machache ambapo alirejea wito wake wa kuwataka vijana hao kuhakikisha wanafanya vizuri kwa kutekeleza maagizo ya makocha wao Jacob Michelsen na Jamhuri Kihwelu huku wakijua wazi kuwa wamebeba roho za watanzania wengi ambao wanawaunga mkono.

Amewata kuiga mfano wake ambapo mbali ya kuichezea timu ya Taifa katika miaka ya sabini na themanini lakini pia alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ambayo ilishiriki kwa mara ya mwisho fainali za mataifa ya Afrika.

Amewataka pia kukumbukuka maneno mazuri aliyozungumza gwiji la zamani la soka barani Afrika Abeid Pele ambaye alikuwepo nchini hivi karibuni ambapo mmoja wa wachezaji wa Serengeti, Hussein Twaha alimnukuu Pele alipozungumza nao uwanja wa Karume pale alipowatembelea maneno ambayo yaliwasisimua wadau waliokuwepo ukumbini hapo.
Alisema , “mpira hauchezwi na watoto wa matajiri bali watoto wa maskini na kipaji pekee hakitoshi kukupeleka kwenye mafanikio bali inahitajika juhudi binafsi” mwisho wa kunukuu.

Kwa upande wake makamu mwenyekiti wa kamati ya Serengeti Kassim Dewji amewataka vijana hao kusahau maneno ya kuwa Congo imekuja na wachezaji vijeba na badala yake wafanye kazi kuhakikisha wanawadhibiti vilivyo na ushindi upatikane.

Dewji amesema yeye anaamini maandalizi waliyofanya vijana hao ni mazuri na kwamba wahakikishe wanatoka na ushindi wa kishindo katika mchezo wa jumapili ili kuwapa kazi ya ziada katika mchezo wa marudiano utakao fanyika nchini Congo wiki mbili baadaye.

Neno zuri kwa vijana hao kutoka kwa Dewji ni kwamba anaamini watavuka hatua hiyo na wataelekea Morroco Mwakani na kwamba baada ya fainali za Morroco basi Mungu akipenda wachezaji zaidi ya 15 watape timu za kucheza barani Ulaya.

Naye Mwenyekiti wa Azam mzee Said Mohamed alikumbushia namna alivyocheza soka wakati wa ujana wake ambapo alisema alikuwa hodari katika kupenyeza mipira ya krosi ambapo alikuwa na uwezo wa kukimbia na kupiga jambo ambalo lilikuwa likimfurahisha kocha wake na hivyo vijana hao waige mfano wake

Juliana Matagi Yasoda, Kaimu Mkurugenzi ya michezo Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo amesema serikali iko nyuma ya vijana hao na kwamba imemshangaza kuona timu ya taifa ya vijana ikifanyiwa hafla nzuri kama hiyo jambo ambalo hakuwahi kuliona siku za nyuma.

Hata hivyo kilio chake ni kwamba wajitume kwa kadri wawezavyo na kwamba serikali inawasapoti.

Jacob na Kihwelu wamewahamasisha vijana kufanyia kazi yale wanayo wafundisha na kwamba wana imani uwezo mkubwa wa kuwafunga Congo wanao.

Jamhuri Kihwelu amesema   kama wanataka kupata mafanikio na maisha mazuri katika maisha yao, basi muda sasa umefika wa kufanya hivyo ambapo endapo watawafunga CongoBrazaville  basi kila mtu atajitokeza kuwachangia zaidi tofauti na ilivyo sasa.

Timu hiyo ya vijana imehashia kambi yake katika hoteli ya JB Belmonte na itaendelea kuwepo hapo mpaka baada ya mchezo wao dhidi ya Congo Brazzaville mchezo ambao utachezwa jumapili katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment