Pages

Saturday, November 17, 2012

BONANZA LA CHANEDA LAFANA

Afisa Michezo Mkoa wa Dar es salaam Adolf Halii akiongea na wachezaji wa netiboli jana kwenye viwanja vya harbours view Kurasini

Baadhi ya wachezaji wa netiboli wakimsikiliza mgani rasmi

Baadhi ya viongozi wapya wa CHANEDA

Timu ya netiboli ya Kilawani yenye blue na

Uhamiaji Queens waliovaa nyeusi wakipambana na wanaume kombaini, Uhamiaji ilichapwa


Wnaume wakionyeshaumahiri wa kucheza netiboli



BONANZA la mchezo wa netiboli lililofanyika kwenye viwanja vya Harbours view Kurasini jana kwa lengo la kutambulisha uongozi mpya wa Chama cha Netiboli mkoa wa Dar es salaam (CHANEDA) lafana.

Bonanza hilo lilishirikisha timu sita na mbili zikiwa za wanaume lilianza saa nane mchana.

Awali akizungumza na wanamichezo na uongozi mpya wa CHANEDA, mgeni rasmi ambaye ni Afisa Michezo wa Mkoa wa Dar es salaam Adolf Halii aliwataka wachezaji kushirikiana na uongozi mpya na yeye atakuwa karibu nao maana hata yeye ni mchezaji wa netiboli.

"Nawapongeza wote mlioshiriki kwenye bonanza hili ila nawaomba mshirikiane na uongozi huu mpya ili tuendeleze michezo Dar es Salaam maana hata mimi nacheza netiboli nafasi ya GS", alisema Halii.

Naye Edson Abubakar anayechezea timu ya wanaume ya Kaza roho ya Kipunguni aliwataka viongozi waanzishe ligi ya netiboli ya wanaume na kusaidia vilabu ili kuvitia moyo.

Timu zilizoshiriki ni Kipunguni Queens ambayo iliifunga Kiwalani 10-3, Karaza roho ambayo iliifunga Majumba sita (wanaume) 16-10, Bandari B iliifunga Kiwalani 18-5 na Wanaume mchanganyiko wakaifunga uhamiaji 11-10.

Uongozi mpya wa CHANEDA uliotambulishwa ni Winfrida Emanuel-Mwenyekiti, Pilly Mogella-Makamu Mwenyekiti, Joseph Ng'anza-Katibu, Christina Kimamla-Katibu msaidizi, Anita Hangoli-Mweka hazina na Mauris Michael-Afisa

No comments:

Post a Comment