Pages

Wednesday, November 28, 2012

SERENGETI BOYS KUKWEA PIPA LEO, KUAGWA HOTELINI ITUMBI SAA 12 JIONI LEO



TIMU ya Taifa ya vijana waliochini ya miaka 17 'Serengeti boys' inaondoka leo usiku nchini kwenda Congo Braza ville kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

Timu hii inaondoka na msafara 27 ikiwa ni wachezaji 18 na viongozi tisa huku wakiwa na matumaini makubwa ya kusonga mbele baada ya mchezo wa awali uliochezwa nchini kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Serengeti boys ambayo imeundwa na wachezaji chipukizi waliopatokana kutokana na mashindano ya Copa Cocacola wanatamani kushinda mchezo ili waweze kuandika historia ambayo haijawahi kuandikwa hapa nchini.

Itakumbukwa kuwa Tanzania iliwahi kufuzu kushiriki fainali hizi 2005 lakini ikaondolewa na ikafungiwa baada ya kugudulika umri wa mchezaji Nurdin Bakari kuwa mkubwa.

Awali jana akizungumza  leo Kocha Mkuu wa timu hii Jakob Michelsen alisema timu yake ipo tayari kupambana na Congo Brazaville na anajivunia faida ya bao moja walilolipata nyumbani.

"Wachezaji wapo kamili na wana ari ya kushinda mchezo huo na kwa sababu nyumbani tulishinda tunaamini tutashinda pia", alisema Jacob

LENZI YA MICHEZO  imeshuhudia mazoezi ya timu hii tangu imalize mchezo wa awali uliochezwa wiki mbili zilizopita na kuona kuwa wachezaji hawana pumzi ya kuhimili dakika 90 japo wana uwezo wa kuchezea mpira.

Kiukweli timu inahitajika kutumia mbinu mbadala kwani mazoezi wanayofanya siku zote ni ya kucheza mpira na siyo kujenga ustahimilivu na pia hali ya hewa ya Congo Braza ville sijui kama inaendana na Dar es salaam.

Kwa mtu yeyote aliyeona mchezo wa nyumbani hatasita kukubali kuwa timu haina pumzi kwani hata mchezo ulipomalizika hawakuweza kushangilia na ni kitu adimu sana kwa timu kushinda na wakashindwa kushangilia.

Tunawatakia kila la heri mfanikiwe kufuzu fainali za vijana zinazotarajiwa kuchezwa nchini MoroccO, Machi mwakani.

No comments:

Post a Comment