Pages

Sunday, November 4, 2012

POLISI YAISWEKA VILLA SQUAD LUPANGO

TIMU ya Polisi Dar es salaam juzi iliifunga Villa Squad mabao 2-1 kwenye mchezo wa ligi daraja kwanza uliochezwa uwanja wa Karume jioni

Polisi ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 20 kupitia kwa Paul Sikazwa bao lililodumu hadi mapumziko.

Timu zote baada ya kutoka mapumziko zilifanya mabadiliko ambayo yaliziongezea uhai na dakika 53 Villa Squad walisawazisha bao kupitia kwa Ally Mrisho


Wachezaji wa Polisi kuona Villa wamesawazisha walisharuka mithili ya askari aliyeona maandamano yasiyo rasmi na kuliandama lango la Villa na dakika ya 60 waliongeza bao kupitia kwa Musiba Joto.


Katika mchezo huo nahonda wa Villa ilimlazimisha Kidamba Omary kukimbizwa hospitali ya Muhimbili na gari la wagonjwa kwa matibabu zaidi baada ya kugongana na Magige Belence wa Polisi dakika ya 12 ya mchezo

Kocha wa Polisi Ulimwengu Hamimu alisema pamoja na kuwa wanashinda, waamuzi wanawaumiza sana kwa kupendelea timu pinzani ila wao wameamua kucheza mpira kwa juhudi zao.

Katika hali isiyo ya kawaida makocha wa Villa Squad Bakari Iddy na Richard Mbuya waligoma kuzungumzia mchezo huo


No comments:

Post a Comment