Pages

Sunday, November 4, 2012

ASHANTI YAZIDI KUNYANYASA KUNDI B

TIMU ya Ashanti United ya Ilala imeendelea kuzinyanyasa timu inazokutana nazo kwenye ligi daraja la kwanza  baada ya juzi kuifunga Green Worriors mabao 2-1, mchezo uliochezwa uwanja wa Mabatini Pwani.

Ashanti ambao wapo kundi B walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za Green Warriors dakika ya 24 kupitia kwa Abdallah Mohamed na Benedict Ngassa dakika ya 47 na wapinzani wao walijipatia bao la kupitia kwa Adam Sadik dakika ya 63.

Kwenye kundi A uwanja wa Majimaji Songea, wenyeji Majimaji waliifunga Burkina Fasso  mabao 3-0, shukrani ya pekee kwa mchezaji Edward Songo aliyepiga hat-trick dakika ya kwanza, 22 na 85.

Kweye uwanja wa Sokoine Mbeya ule mchezo ambao ulishindikana kuendela kutoka na mvua kubwa iliyonyesha na kusababisha uwanja kujaa maji ulirudiwa juzi asubuhi na matokeo yake Mbeya City ilishinda kwa mabao 3-0.

Mchezo huo ulishindikana kuendelea zikiwa salia dakika 45 na mpaka unasimama Mbeya City walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0.

Mabao yalifungwa na Fidelis Castory dakika ya 14 na Hassan Mwasapili dakika ya 34 na Innocent Bony dakika ya 85

Huko Kiteto wenyeji Moran walitoshana nguvu na Polisi Tabora ya bao 1-1 ambao ni mchezo wa kundi C.

No comments:

Post a Comment