Pages

Saturday, October 20, 2012

YANGA YAIFUNGA RUVU SHOOTING 3-2









TIMU ya Yanga leo imeshinda 3-2 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huu unaifanya Yanga ifikishe pointi 14, baada ya kucheza michezo nane na kujiweka katika nafasi ya tatu huku ikizidwa pointi tatu na Azam inayoshika nafasi ya pili na pointi nne na wapinzani wao wa jadi Simba inayoongoza ligi hiyo.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu zote kutoshana nguvu kwa mabao 2-2, Ruvu Shooting wakitangulia kufunga na kusawazisha.

Mabao ya Ruvu yalifungwa na mshambuliaji Seif Abdallah dakika ya tatu na lingine dakika ya 10.

Mabao ya Yanga yalifungwa na Mbuyi Twite dk 20 baada ya Rashid Gumbo kufanyiwa faulo nje ya eneo penalti na bila ajizi beki huyo wa Yanga aliyetokea APRkupiga shuti kali lililomshinda golikipa Benjamin Haule.

Jeryson Tegete alifunga bao la pili baada ya kuunganisha krosi nzuri aliyopiga Juma Abdul dakika ya 36.

Bao la tatu lilifungwa dk 65 na Didier Kavumbagu kipindi cha pili.

Baadae Ruvu shooting walizinduka na kufanya mashambulizi ambayo yalisababisha kosa kosa langoni mwa Yanga lakini bahati haikuwa yao kwan mpaka mwamuzi anapuliza filimbi ya kumaliza mchezo mabao yalikuwa 3-2

Kikosi cha Yanga ni; Yaw Berko, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Rashid Gumbo, Nurdin Bazkari, Haruna Niyonzima, Jerry Tegete, Didier Kavumbangu na David Luhende.

Ruvu Shooting; Benjamin Haule, Michael Aidan, Baraka Jaffari, George Assey, Ibrahim Shaaban, Ernest Ernest, Raphael Kyala, Hassan Dilunga, Seif Abdallah, Abrahman Mussa na Said Dilunga.

Kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Mkwakwani, Tanga, Coastal Union imeifunga Mtibwa Sugar mabao 3-1, wafungaji wa Coastal Union ni Juma Jabu, Daniel Lyanga na Lameck Dayton huku la Mtibwa likifungwa na Shaaban Nditi.

No comments:

Post a Comment