Pages

Friday, October 19, 2012

BOBAN KUIKOSA MGAMBO JKT JUMAPILI




BOBAN
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Haruna Moshi 'Boban' na beki wa kati wa timu hiyo, Juma Nyosso wametemwa katika kikosi cha timu hiyo.

Boban ameshindwa kwenda mkoani Tanga, ambako jumapili watacheza na Mgambo Shooting, kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, kutokana na kukabiliwa na maumivu ya misuli.

Timu hiyo iliyoondoka Dar es Salaam leo, ikiwa na wachezaji 24, Nyosso alimeondolewa katika kikosi kitakachocheza jumapili kutokana na anakadi tatu za njao.

Ofisa Habari wa Klabu hiyo, Ezekiel Kamwaga alisema leo  kuwa  wachezaji  waliobaki Dar es Salaam ni Shomari Kapombe, Haruna Shamte na Kigi Makasi ambao ni majeruhi.

Wachezaji waliondoka ni Juma Kaseja, Wilbert Mweta, Waziri Hamad, Nassor  Masoud 'Chollo', Amir Maftah, Paulo Ngalema, Koman Bili Keita, Pascal Ochieng, Hassan  Kondo na Jonas Mkude.

Wengine ni Ramadhani Chombo 'Redondo', Amri Kiemba, Abdallah Seseme, Ramadhani Singano, Uhuru Selemani, Mrisho Ngassa, Mwinyi Kazimoto, Salim  Kinje, Abdallah Juma, Daniel Akuffo, Felix Sunzu, Edward Christopher, Haruna Athumani na Emmanuel Okwi

Wakati huo huo, Kocha wa timu hiyo,  Milovan Cirkovic amesema  baada ya kupoteza pointi sita kutokana na kutoka sare katika mechi tatu kikosi chake kipo fiti katika mchezo huo.

Cirkovic alisema matokeo hayo ya sare hayamaanishi timu yake ni mbovu ila mashabiki wanatakiwa kuondoa wasiwasi juu ya kiwango cha timu yao.

Alisema kupoteza pointi sita sio tatizo  ila ni matokeo ya mchezo, kwani hakuna timu inayokwenda uwanjani kwa lengo la  kufungwa.

Wakati huo huo, Uongozi wa klabu hiyo  imesema unatarajia kuliweka kitimoto benchi la ufundi kutokana na mwenendo wa timu hiyo kutoka sare mfululizo.

Makamu mwenyekiti wa klabu hiyo, Geofrey Ngange 'Kaburu' alisema kutokana na ushindani wa ligi hiyo, matokeo hayo ni mabaya kwa upande wao kwani wanatakiwa kushinda la sio kutoka sare.

Kaburu alisema baada ya kushindwa kuifunga Coastal Union na Kagera Sugar, wanaelekaza nguvu katika mchezo wa Jumapili dhidi ya Mgambo ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi

No comments:

Post a Comment