Pages

Wednesday, October 3, 2012

SIMBA NA YANGA ZATOKA SARE


SIMBA na YANGA zimetoka sare ya 1-1 kwenye mchezo wa ligi uliochezwa uwanja wa Taifa usiku jana.
 
Yanga ambao ilibidi walazimishe sare ya kufungana bao 1-1 na wapinzani wao wa jadi kwani walionekana kutocheza vizuri walimaliza mechi wakiwa pungufu baada ya Simon Msuva kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 77 kwa kumpiga Juma Nyosso wakati mpira ukiwa hauko mchezo, ndio waliohaha kusawazisha bao, baada bao la mapema la kiungo Amri Kiemba.   

Simba walicheza vizuri kipindi chote cha kwanza wakipigiana pasi za uhakika na kuwazidi kasi wapinzani wao.   

Kwa matokeo hayo, Simba imefikisha pointi 13, ndani ya mechi tano na kuendelea kuongoza Ligi Kuu, wakati Yanga imefikisha pointi nane na kubaki nafasi ya tano, kwani Coastal Union imetoa sare ya 2-2 na JKT Oljoro mjini Arusha na kufikisha pointi tisa.    

Amri Kiemba akishangilia bao alilofunga dakika ya 6

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao alilofunga Amri Kiemba

Mshambuliaji wa Simba Mrisho Ngasa akiachia shuti

Wachezaji wa Yanga wakishangilia baada ya Bahanunzi kusawazisha bao kwa njia ya penalti

Mashabiki wa Yanga wakionyesha vibweka katika kushangilia

Shabiki wa Simba akishangilia kwa staili yake huku usalama ukiwa umeimarishwa

No comments:

Post a Comment