Pages

Saturday, October 6, 2012

SIMBA ITAENDELEZA UBABE LIGI KUU LEO?






 



LEO uwanja wa taifa jijini Dar es salaam Simba watakuwa wenyeji wa JKT Oljoro mchezo utakaochezwa majira ya saa kumi jioni.

Simba ambao wanafanya mazoezi uwanja wa Kinesi wanasema watafanya vizuri mchezo huo waendelee kulinda heshima kwani mpaka sasa hawajafungwa hata mchezo mmoja zaidi ya sare ya juzi na Yanga.

Michezo mingine itakayochezwa hapo leo ni Mgambo JKT ambao wanawakaribisha Polisi Morogoro mchezo utakaochezwa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Toto African wao wanaialika JKT Ruvu ya Pwani kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza
Prison ya Mbeya "wajelajela" wanawakaribisha wakata miwa wa Turiani "Mtibwa Sugar" kwenye dimba la Sokoine mjini Mbeya 


















No comments:

Post a Comment