TIMU ya Simba ya Dar es salaam leo mchana imeondoka kwenda Tanga kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Octoba 13 uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Simba ambao wamepanda basi lao walililopewa na wadhamini wao kampuni ya Bia Tanzania (TBL) imeondoka bila mshambuliaji wao wa Kimataifa wa Uganda Emanuel Okwi ambaye ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda.
Wengine ambao hawakufuatana na timu ni Ramadhan Chombo Redondo ambaye anasumbuliwa na malaria,Haruna Shamte, Hamadi Waziri na Komabil Keita ambao ni majeruhi.
Kamwaga alisema Mrisho Ngassa aliyekuwa anaumwa malaria amepona na yupo kwenye msafara utakaondoka leo na nyota wengine ambao siyo majeruhi
No comments:
Post a Comment