Pages

Thursday, October 11, 2012

KOCHA ASHANTI UNITED ASEMA HANA HOFU NA KIKOSI CHAKE

Wachezaji wa Ashanti wakiwa mazoezini




KOCHA wa Ashanti United inayoshiriki ligi daraja la kwanza Mubaraka Hassan amesema kikosi chake kipo vizuri na kamwe haofii timu yoyote iliyopo kwenye kundi lao.

Akizungumza na BINGWA juzi jioni akiwa mazoezini uwanja wa Rovers, Msimbazi Centre alisema kikosi chake kipo vizuri na hana na wasiwasi na timu walizopangwa nazo kundi moja kwani watafanya vizuri.

Ligi daraja la kwanza ambayo imepangwa katika makundi matatu yenye timu nane nane inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Octoba 20 kwa mtindo wa kucheza nyumbani na ugenini na kila kundi litatoa mshindi mmoja ambaye ataingia ligi kuu.

Ashanti ambayo imepanda daraja la kwanza msimu huu imepangwa kundi B moja na timu za Ndanda FC ya Mtwara, Green Warriors, Moro United, Polisi, Tessema, Transit Camp na Villa Squad zote za Dar es Salaam.

Pia kocha huyo alisema kuwa anajivunia wachezaji chipukizi alionao na inaimani watafanya vizuri ili waendeleze sifa ya Ashanti ya kutoa wachezaji wenye vipaji na uwezo kama akina Juma Nyosso, Adam Kingwande na wengine wengi.

Mazoezi ya Ashanti yanayofanyika kila siku jioni uwanja wa Rovers Msimbazi Center yanauhudhuriwa na mashabiki wengi wa Ilala.

No comments:

Post a Comment