Pages

Monday, October 29, 2012

SHIREFA YAPATA UONGOZI MPYA

CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Shinyanga (SHIREFA) kimepata uongozi mpya kupitia uchaguzi uliofanyika Oktoba 27 mwaka huu.

Viongozi waliochaguliwa ni Benester Lugora ambaye ni Mwenyekiti, Nassoro Said, Katibu Mkuu, Bivin Kapufi, Katibu Msaidizi, Mbasha Matutu, Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF na Michael Kaijage ambaye ni Mwakilishi wa Klabu TFF.

Pia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya na kamati iliyosimamia uchaguzi huo kwa kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa mujibu wa kanuni.

Taarifa iliyotuma kwa vyombo vya habari inasema kuwa Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa SHIREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Shinyanga.

TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya SHIREFA ambayo imechaguliwa chini ya uenyekiti wa Benester Lugora.

Pia uongozi mpya una changamoto nyingi ya kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu Shinyanga kwa kuzingatia katiba ya SHIREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake

No comments:

Post a Comment