Pages

Monday, October 29, 2012

LIGI YA DAYOSA< MSIMAMO YAINYUKA NGWELE 5-0

Mchezaji wa Ngwele akijaribu kuwazuia wachezaji wa Msimamo kwenye mchezo uliochezwa jana uwanja wa Karume



Mchezaji wa Msimamo aliyevaa jezi nyekundu akikokota mpira huku mchezaji wa Ngwele akimkimbiza
TIMU ya vijana walio chini ya mika 17 Msimamo inayoshiriki ligi ya vijana jana waliwafunga Ngwele mabao 5-0 kwenye mchezo uliochezwa juzi asubuhi uwanja wa Karume.

Ligi hiyo ambayo inaendeshwa na chama cha kukuza vipaji Mkoa wa Dar es Salaam (DAYOSA)ilishuhudia vijana waliojaa vipaji wa Msimamo wakiibugiza bila huruma Ngwele.

Mabao kupitia kwa Dunia Seleman dakika ya saba, Mfaume Fikiri dakika ya 11, 25 na 26 na karamu ilihitimishwa na Mfaume Fikiri dakika 56 kipindi cha pili.

Msimamo wanaofundishwa na kocha Hatibu Ally, alisema timu yake ipo vizuri na ushindi walioupata walistahili pia akawapongeza wachezaji kwa kufuata alichowafundisha.

Mchezo mwingine Abba  walipata ushindi wa chee wa pointi tatu na mabao 2 baada ya Palest kuchelewa kufika uwanjani.

Akizungumza jijini mratibu wa mashindano hayo Mohamed Tambaza alisema wameandaa mashindano hayo ili waendeleze vipaji vya wachezaji wanaochipukia.

Pia alizitaka timu zote zianzishe timu B za vijana ili kuwe na timu bora ya baadae badala ya kuendelea kununua wachezaji toka nje kwa bei ghali 
"Timu zetu zinanunuwa wachezaji kwa bei ghali badala ya kuwekeza kwenye soka la vijana ili kujenga timu bora za baadae", alisema Tambaza.

No comments:

Post a Comment