Pages

Tuesday, October 16, 2012

RATIBA DARAJA LA KWANZA HADHARANI

Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ya Tanzania Bara inaanza rasmi Oktoba 24 mwaka huu badala ya octoba 20 iliyotangazwa awali  kwa timu 18 kati ya 24 kujitupa kwenye viwanja tisa tofauti katika ligi hiyo inayochezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
 
Akizungumza na waandishi wa habari ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema mechi za raundi ya kwanza za kundi A zitakazochezwa Oktoba 24 mwaka huu ni Burkina Faso dhidi ya Mbeya City uwanja wab Jamhuri, Morogoro, Mlale JKT na Small Kids uwanja wab Majimaji, Songea na Kurugenzi Mufindi dhidi ya Majimaji, uwanja wa Wambi, Mufindi mkoani Iringa.
 
Mkamba Rangers na Polisi Iringa zitakamilisha raundi ya kwanza kwa kundi hilo Oktoba 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
 
Mechi za raundi ya pili kwa kundi hilo zitachezwa Oktoba 27 mwaka huu kwa Polisi Iringa vs Mbeya City uwanja wa Samora, Iringa, Majimaji vs Small Kids uwanja wab Majimaji, Songea, Burkina Faso vs Mkamba Rangers uwanja wa Jamhuri, Morogoro na Kurugenzi Mufindi vs Mlale JKT  uwanja wa Wambi, Mufindi.
 
Raundi ya tatu ni Oktoba 31 mwaka huu kwa mechi kati ya Mbeya City vs Mlale JKT uwanja wa Sokoine, Mbeya, Small Kids vs Mkamba Rangers  uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga, Majimaji vs Burkina Faso uwanja wa Majimaji, Songea na Polisi Iringa vs Kurugenzi Mufindi uwanja wa Samora, Iringa.
 
Kundi B Oktoba 24 mwaka huu ni Ndanda vs Transit Camp, uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, Villa Squad vs Moro United, uwanja wa Mabatini, Pwani, wakati Oktoba 25 mwaka huu ni Green Warriors vs Tessema uwanja wa Mabatini, Pwani  na Polisi Dar es Salaam vs Ashanti United uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
 
Raundi ya pili kwa kundi hilo ni Oktoba 27 mwaka huu Ndanda vs Green Warriors wa Nangwanda Sijaona, Mtwara, Villa Squad vs Tessema uwanja wa Mabatini, Pwani wakati Oktoba 28 mwaka huu ni Ashanti United vs Transit Camp  uwanja wa Mabatini, Pwani na Oktoba 29 mwaka huu ni Moro United vs Polisi Dar es Salaam uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.
 
Novemba 1 mwaka huu ni Green Warriors vs Ashanti United uwanja wa  Mabatini, Pwani, Novemba 2 mwaka huu ni Polisi Dar es Salaam vs Villa Squad uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam,  Novemba 4 mwaka huu ni Tessema vs Ndanda wuwanja wa Chamazi, Dar es Salaam na Transit Camp vs Moro United uwanja wa Mabatini, Pwani.
 
Kundi C ni Oktoba 24 mwaka huu Kanembwa FC vs Polisi Dodoma uwanja wa  Lake Tanganyika, Kigoma, Mwadui vs Morani uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Pamba vs Polisi Mara  uwanja wa Kirumba, Mwanza na Rhino Rangers vs Polisi Tabora  wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora.
 
Raundi ya pili ni Oktoba 27 mwaka huu; Polisi Tabora vs Polisi Dodoma uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora, Mwadui vs Polisi Mara uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Kanembwa FC vs Morani uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma na Pamba vs Rhino Rangers uwanja wa Kirumba, Mwanza.
 
Oktoba 31 mwaka huu ni raundi ya tatu; Polisi Mara vs Rhino Rangers uwanja wa Karume, Musoma, Morani vs Polisi Tabora uwanja wa Kiteto, Manyara, Polisi Dodoma vs Pamba uwanja wa Jamhuri, Dodoma na Kanembwa FC vs Mwadui uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.

No comments:

Post a Comment