Pages

Tuesday, October 30, 2012

POLISI YAICHEZESHA MORO UNITED KWATA KARUME

Kikosi cha Polisi Dar es salaam

Waamuzi wakiingia uwanjani



Kocha wa Moro United Yusuph Macho akiwa na wenzake kwenye benchi la ufundi


Baada ya Nsa Job kuumia Chamazi na kukosekana gari la wagonjwa  hatimaye TFF waleta Ambulance kwenye ligi daraja la kwanza

TIMU ya Polisi ya Dar es Salaam jana iliifunga Moro United mabao 3-2 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Karume jijini Dar es salaam.

Polisi ambao mchezo uliopita walifungwa na Ashanti United juzi ilijipatia mabao yake kipindi cha kwanza kupitia kwa Henrico Kayombo kwa njia ya penalti baada ya mshambuliaji Benjamini Peter kuangusha eneo la penalti dakika ya 26, Magige Belence dakika ya 34 na Julias Mrope alipigilia msumari wa mwisho dakika ya 39.

Baada ya kutoka mapumziko Moro United ilizinduka  na kulishambulia lango la Polisi na kujipatia mabao yake kupitia kwa Orafu Mwamlima kwa njia ya penalti dakika ya 77 baada ya beki kushika mpira eneo la penalti na Madafa Nyange dakika ya 80.

Kocha wa Polisi Dar es salaam Ngero Nyanjaba aliwatupia lawama wachezaji wake kuwa wanajisahau sana kwenye mchezo zinapofika dakika za mwishoni kwani hata Ashanti iliwafunga kwenye dakika za mwishoni.

"Wachezaji wangu wanacheza vizuri lakini wanajisahau sana zinapofikia dakika za mwishoni ndio tunafunga kitu ambacho naweza kusema tunajifunga wenyewe", alisema

Naye Yusuph Macho kocha wa Moro United alisema kuwa timu yake ilistahili ushindi lakini umakini wa mabeki na washambuliaji umesababisha wapoteze mechi kwani hata mchezo uliopita walifungwa.

No comments:

Post a Comment