Pages

Tuesday, October 30, 2012

BFT YATEUA WAAMUZI WA KUCHEZESHA MPAMBANO WA TANZANIA NA ZAMBIA

SHIRIKISHO la ngumi Tanzania (BFT) limeteuwa waamuzi 10, watakaochezesha mashindano ya kirafiki ya kimataifa na kwa kushirikiana na mmoja atakayetoka Zambia


Akizungumza na Wanahabari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa BFT Makore Mashaga alisema kuwa mashindano hayo yatafanyika Novemba 3 mwaka huu, saa 9.00 alasiri katika ukumbi wa DDC kariakoo.

Aliwataja wamuzi walioteuliwa kuwa ni wa ngazi Za kitaifa na kimataifa ambao ni
Mohamed Kasilamatwi, Juma Selemani (Wote AIBA) Maneno Omari, Ridhaa Kimweli, Mohamed Bamtula, Michael Mwankenja, salehe Mwinyikheri na  Caesar Musuka  kutoka  Zambia hao ni wa ngazi ya kitaifa wakati madaktari Daniel  Mashaga, Joseph Magesa.

Mashaga alifafanua kuwa waamuzi hao pamoja na madaktari wameteuliwa kutokana na utendaji wao usio na shaka katika mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.

Pia amewataka watanzania  kuhudhuria kwa wingi kushangilia mabondia wao siku hiyo ili wapate moyo wa kujituma zaidi.

"Natoa wito kwa Watanzania wenzangu wajitokeze kwa wingi ili kuwashangilia mabondia wetu waweze kufanya vyema katika mashindano hayo," alisema.

No comments:

Post a Comment