Pages

Monday, October 29, 2012

NSA JOB HAKUVUNJIKA



Nsa Job akiwa amelala kitandani hospitali ya Muhimbili baada ya kufungwa bandeji ngumu (POP)

UONGOZI wa klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga, amewatoa hofu mashabiki kuwa Nsa Job  anaendela vizuri baada ya kugundulika kuwa hakuvunjika goti wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu, kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar es Salaam Jumapili iliyopita.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ahmed Aurora alisema kuwa wamefarijika baada ya kupata taarifa za kitabibu toka kwa madaktari wa hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo amelazwa, zinaweka wazi kuwa Nsa Job hakuvunjika ingawa goti  lake bali liligeuka  lakini kwa sasa limerudishwa kwenye hali yake ya kawaida na kufungwa bandeji gumu (P.O.P).

Pia alisema kuwa katika mazingira hayo imekuwa ni faraja kubwa kwamba mshambuliaji huyo anaweza kurejea uwanjani ndani ya muda mfupi tofauti walivyokuwa wanatarajia.

“Madaktari wametudhibitishia kuwa hali yake inaendelea vizuri baada ya kugundulika kuwa hakuvunjika goti ila liligeuka na kuwa nje ya njia yake ya kawaid hivyo  imerudishwa na sasa anaendekea vizuri.

“Ni imani yetu kubwa kwamba atarejea kwenye hali yake ya kawaida baada ya muda mfupi kutoka sasa kufuatia matibabu aliyopewa,” alisema Aurora.
Pamoja na matokeo hayo mazuri ya mabao 3-0 kikosi chake iliyopata dhidi ya maafande wa JKT Ruvu, mashambuliaji huyo alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuumia kufuatia kukosa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) kwenye uwanja huo hivyo kupelekwa hospitali kwa usafiri wa kuunga unga. 

Nsa Job ambaye ni nyota wa zamani wa timu za Yanga na Villa Squad zote za jijini Dar es Salaam aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya Coastal Union na JKT Ruvu ambapo mashabiki wengi wa soka walilaani kukosekana kwa ambulance hiyo ambayo ni moja ya huduma kuhimu.

No comments:

Post a Comment