TIMU ya Coastal Union ya Tanga leo imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga JKT Ruvu mabao 3-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Chamazi, Mbande Dar es salaam.
JKT Ruvu ambao walikuwa wenyeji walijikuta wakipokea kichapo hicho kipindi cha pili kupitia kwa Danny Lyanga aliyefunga mabao mawili na Said Swed.
Hata hivyo ushindi wa Coastal Union uliingia dosari baada ya mchezaji Nsa Job kuumia na amelazwa hospital ya Muhimbili baada ya kuruka na kugongana na mchezaji mwenzake na kuumia
Binafsi nampa pole apone haraka ili arudi tena dimbani kuendeleza kipaji chake na Mungu amsaidie. Amina
No comments:
Post a Comment