Pages

Monday, October 15, 2012

MWAMUZI ODEN MBAGA KUZICHESHA KENYA NA AFRIKA YA KUSINI KWENYE UWANJA WA NYAO NAIROBI

Mwamuzi wa kimataifa Oden Mbaga (aliyevaa jezi ya light blue) Idd Maganga (katikati)  Jamhuri na aliyekaa chini ni Omari Miyala  kwenye uwanja wa Taifa hivi karibuni


MWAMUZI wa kimataifa wa Tanzania Oden Mbaga amechaguliwa kuchezesha mchezo wa kirafiki kati ya Kenya na Afrika ya Kusini mchezo utakaochezwa kesho kwenye uwanja wa Moi Kasarani.

Mbaga atasaidiwa waamuzi wasaidizi John Kanyeye na Jese Erasmo wote wa Tanzania.

Mchezo huo ni wa kirafiki kutokana na ratiba ya Shirikisho la kimataifa kuagiza nchi wanachama kucheza mechi za kirafiki kila mwezi. 
TFF imeteua waamuzi hao baada ya kupata maombi kutoka kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kenya (FKF) ambao ndiyo waandaaji wa mechi hiyo ambayo ni moja ya vipimo kwa kocha mpya wa Harambee Stars, Henry Michel kutoka Ufaransa

Pamoja na kuwa mashabiki wa soka Tanzania wamekuwa wakiwatuhumu waamuzi bila kuelewa sheria wameendelea kupata michezo ya kimataifa. kwa nchi zingine kuwaona bora sana kuliko walio nao



No comments:

Post a Comment