Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, October 26, 2012

DIDIER KAVUMBAGU: YANGA UBINGWA NI WETU



MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Yanga, Didier Kavumbagu amesema wataendelea kuwapa raha mashabiki wao kwa kushinda mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana kabla ya kuondoka kwenda Arusha Kavumbagu alisema ili waweze kufikia lengo la kuchukua ubingwa wanaiona kila mechi kwa ni fainali na wanatakiwa kushinda.

Kavumbagu alisema ushindani wa ligi hiyo, umekuwa ni mkubwa hivyo, wachezaji wenzake wanatakiwa kujituma zaidi.

Alisema pamoja na kuanza vibaya  katika ligi hiyo, hawatakata tamaa kutokana na wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

Kavumbagu alisema matokeo mabaya wanayapata hasa wanapokuwa katika mechi za ugenini na yanasababisha na waamuzi.

Alisema baadhi ya waamuzi wanaochezesha mechi zao za ugenini hawazingatii sheria 17, kutokana na wanakuwa na maamuzi ya upande mmoja.

“Waamuzi wanachezesha sivyo kabisa ndio maana wanalalamikiwa sana,” alisema Kavumbagu.

Kavumbagu aliyesajiliwa na klabu hiyo msimu huu, akitokea Atletico ya Burundi ameifungia Yanga mabao matano tangu ilipoanza ligi hiyo, Septemba 15, mwaka huu.

Timu hiyo, ambayo juzi iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Polisi Morogoro, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam,  ilitarajia kuondoka jana kwenda Arusha, ambako kesho itacheza na JKT Oljoro, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

No comments:

Post a Comment