Pages

Wednesday, September 19, 2012

TIMU ZA NGUMI ZA MAJESHI ZAFANYA VIZURI MASHINDANO YA TAIFA

BONDIA Seleman Bemtula wa Magereza juzi jioni alimtwanga Joseph Peter wa Pwani kwa pointi kwenye mashindano ya ngumi za ridhaa ya Taifa.

Mabondia ambao walikuwa wanapambana kwenye mchezo wa raundi tatu kg 64 walionyeshana ubabe kwa kurushiana makonde mazito huku kila mmoja akishangiliwa na wenzake.

Akizungumzia mashindano hao Katibu wa ngumi za ridhaa Makore Mashagi alissema anashukuru mwaka huu msisimko umeonekana kwa mabondia wenyewe na mashabiki walihudhuria ila tatizo ni kuwa chama kinakabiliwa na ukata mkubwa katika kufanikisha mashindano hayo.

"Nashukuru mashindano yana msisimko maana mikoa imeleta washiriki wengi ila chama kinakabiliwa na ukata kwani bajeti ya mashindano haya mpaka sasa tumefanikisha asilimia nane tu", alisema Makore

Pia amewataka watu na makampuni mbalimbali kujitokeza kuwasaidia ili kufanikisha mashindano hayo ambayo yanashirikisha mikoa 19 baadhi ikiwa na time za kike na kiume ambaye yanatarajiwa kufika tamati Septemba 22 mwaka huu.

Mabondia wengine waliopanda ulingoni ni kg 64 ni Mohamed Mtibwa (Morogoro) ambaye alimpiga Bakari Simfukwe (Kilimanjaro) kwa pointi na Salum Khamis (Tabora) ambaye alimpiga Pascal Martine (Mbeya) kwa pointi pia.

Walipanda ulingoni kg 52 ni Osward Chaula wa Magereza ambaye alimpiga kwa pointi Issa Beleche wa Kilimanjaro, Sunday Elias wa Pwani pia alishinda kwa pointi kwa kumpiga Ally Bob wa Ruvuma, Boniface Mlingwa wa JKT alimpiga kwa pointi Cosmas Peter wa Dodoma.

Pia Abdallah Kassim wa Ngome alimdunda kwa poindi bondia Haidan Mwanga wa Ilala na James Sitaha alishinda baada ya mwamuzi kukatisha mchezo kumnusuru bondia Matata Berard wa Arusha baada ya kuona anazidiwa na makonde (RSCO).

Naye Joseph Meshack wa Arusha alimshinda Fadhili Hassan wa Pwani kwa pointi, Said Hofu wa JKT alishinda baada ya mwamuzi kusimamisha mchezo kwa kuona Emanuel Mogella amezidiwa (RSCO) pia Hemed Salum alipata ushindi wa chee baada ya mpinzani wake Halili Mnyani wa Morogoro kushindwa kutokea ulingo.

Kwa tathimini ndogo iliyofanywa na HABARI ZA MICHEZO imeonekana timu za zinazomilikiwa na taasisi zinaongoza baada ya michezo kumi iliyochezwa juzi kuonekana zimeshinda michezo mitano.



No comments:

Post a Comment