Pages

Wednesday, September 19, 2012

SIMBA YANG'ARA, YANGA YALALA KWA MTIBWA

Wachezaji wa Simba wakishangilia bao alilofunga Amri Kiemba

Mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi akitoka uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu

Mshambuliaji wa Simba Daniel Akuffo  akikimbia na mpira sambamba mchezaji wa JKT Ruvu kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa leo uwanja wa Taifa.        


TIMU ya Simba ya Dar es salaam leo imeifunga JKT Ruvu bao 2-0 kwenye mchezo wa ligi kuu uliochezwa uwanja wa TAIFA ukiwa ni mchezo wa pili kwa kila timu kwenye mzunguko wa pili.

Mabao ya Simba yalifungwa na Amri Kiemba na Haruna Moshi "Boban" kipindi cha pili.
Mchezo ulikuwa ni mzuri sana na mwamuzi Andrew Shamba wa Pwani aliweza kuumudu mchezo vilivyo akisaidiwa na wasaidizi wake Abdallah Selega na Samson Kobe na mezani akiwepo mwamuzi wa kimataifa Oden Charles Mbaga.

Kipindi cha kwanza mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi alionyeshwa kadi nyekundu kwa kumpiga kiwiko wakati mchezo ukiwa haupo mchezo, hivyo kwa kadi hii Okwi atakosa michezo miwili.

Huko Morogoro uwanja wa Jamhuri Yanga ya Dar es salaam wamefungwa bao 3-0 na Mtibwa sukari yenye makazi yake Turiani.

Jijini Mbeya uwanja wa Sokoine Prison ya Mbeya wametoshana nguvu na Coastal Union kwa kutoka suluhu 0-0

Pia jijini Mwanza kwenye uwanja wa CCM Kirumba nako mchezo wa Toto African na Azam aka wauza Ice cream au lambalamba wametoka sare  1-1

Mjini Kibaha kwenye uwanja wa Mabatini Ruvu shooting wameifunga timu iliyopanda daraja msimu huu JKT Mgambo ya Tanga bao 2-0

Kwenye uwanja wa Chamazi wenyeji wa uwanja huo African Lyon wameutumia uwanja wao vema kwa kuifunga Polisi Moro 1-0 , huku timu zote zikikosa penalti

Mjini Bukoba kwenye uwanja wa Kaitaba Kagera Sugar  wametoka suluhu ya 0-0 na JKT Oljoro

Ligii itaendelea tena Septemba 22 mwaka huu kwa michezo minne ambapo Yanga watakuwa uwanja wa Taifa wakiwakaribisha JKT Ruvu ya Pwani

Azam wataikaribisha Mtibwa kwenye uwanja wao uliopo Chamazi na JKT Oljoro wataikaribisha Polisi ya Morogoro kwenye uwanja wa Sheikh Aman Karume jijini Arusha na mchezo mwingine utakuwa ni kati ya Coatal Union na Toto African uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga



No comments:

Post a Comment