Pages
▼
Wednesday, September 19, 2012
AFRICAN LYON WAAPA KUIADABISHA POLISI MORO
KOCHA wa African Lyon Pabio Velez amesema leo kikosi chake kipo tayari kuchukua pointi tatu za mchezo wao na Polisi Moro utakaochezwa uwanja wa Chamazi.
Muagentina huyo alilipasha HABARI ZA MICHEZO kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanashinda mchezo kwani wanataka msimu huu washike nafasi za juu za ligi ya Tanzania.
Pia alisema wanaiheshimu sana Polisi Morogoro na kwa vile ndio wamerudi kwenye ligi watakuwa wanacheza kuhakikisha wanashinda ila na wao wanataka wapate pointi tatu za mchezo huo.
Akizungumzia mchezo wao na Simba anasema walifungwa kwa sababu kwanza kitendo cha wachezaji kuvuliwa jezi zenye nembo ya mfadhili kiliwachanganya kwa muda lakini baadae walirudi kwenye mchezo, pia wachezaji wa nafasi ya kiungo walishindwa kumiliki mpira ndio maana Simba waliwachezea sana kipindi cha kwanza.
"Kitendo cha kuvulia jezi za mdhamini wa timu kiliwachanganya wachezaji lakini pia nafasi ya kiungo ilishindwa kumiliki mpira na Simba kutumia nafasi hiyo kutushambulia" alisema Pablo Velez.
Nao wchezaji wamesema wana ari na mchezo wa leo na watahakikisha wana cheza kufa na kupona kuhakikisha wanashinda.
No comments:
Post a Comment