Pages

Saturday, September 29, 2012

SERENGETI IPO TAYARI KUIVAA MISRI

Wachezaji wa timu ya taifa ya vijana waliochini ya miaka 17, Serengeti boys wakifanya mazoezi
KOCHA wa timu ya Taifa ya vijana waliochini ya umri wa miaka 17 'Serengeti Boys' Jakob Michelsen amejigamba kutoa kipigo cha 'paka mwizi' dhidi ya wenzao wa Misri katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za vijana utakaochezwa Oktoba 14, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Serengeti iliingia katika hatua ya pili ya michuano hiyo baada ya Kenya kujiondoa.

Akizungumza na HABARI ZA MICHEZO jana Michelsen alisema timu hiyo imeiva kwa ajili ya mchezo huo, baada ya kufanya maandalizi kwa muda mrefu.

Michelsen amesema kutokana na maandalizi ya timu hiyo ana imani itaibuka na ushindi ili iweze kujiweka katika mazingira ya kusonga mbele.

Alisema timu hiyo imekaa pamoja kwa muda mrefu baada ya kupata ushiriano kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na wadau mbalimbali.

Timu imecheza michezo tisa ya kirafiki na kushinda nane huku ikifungwa mmoja wakati ikiwa kwenye Kanda ya nyanda za juu Kusini.

Wakati huo huo, wachezaji watatu ni Shiza Ramadhan, Tumaini Baraka na Abdul Seleman wameongezwa katika kikosi hicho ili kuongeza nguvu baada ya kufanya vizuri kwenye mashindano ya copa coca cola yaliyofanyika Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment