Pages
▼
Monday, September 17, 2012
BHARESSA APITISHWA KUWA MGOMBEA
MWENYEKITI wa DRFA Amin Bharessa amepitishwa tena kutetea nafasi yake kwenye uchaguzi ujao licha ya kuwa hana sifa kulingana na katiba ya Shirikisho la Soka nchini.
Akisoma majina yaliyopitishwa na kamati M/kiti wa kamati hiyo Alhaj Muhidin Ndolanga alisema waliopitishwa kugombea nafasi ya M/kiti ni Amin Bharessa na Mchaki
Makamu m/kiti ni Gung'ulwa Tambaza na nafasi ya katibu ni Msanifu Kondo, Said Tulli na Ambali wakati mweka hazina ni Ally Hassan, nafasi za ujumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ni Shafii Dauda na Muhsin Balhboo na ujumbe wa uwakilishi wa vilabu ni Mohamed Bhinda na Benny Kisaka.Hamisi Kisiwa na Sunday Mwanahewa wao wanagombea nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji
Wagombewa walioenguliwa na kamati hiyo kwa kukosa sifa za uzoefu wa miaka mitano wa kuongoza soka kwa nafasi ya Mwenyekiti ni Evans Aveva, Salum Mkemi na Juma Jabri na Salum Mwang'inda anayegombea nafasi ya makamu m/kiti.
Ndolanga alipoulizwa juu ya Bharessa kuwepo ili hali hana elimu ya sekondari alisema kama mtu hajaridhika anatakiwa kukata rufaa maana wao wametumia katiba ya DRFA kupitisha majina hayo.
"Kwa mujibu wa ratiba ya kuelekea kwenye ya uchaguzi huo, leo Septemba 16 ni siku kuweka pingamizi na mwisho wa kamati ya uchaguzi kupokea pingamizi ni Septemba 20 saa 10 alasiri.
Hakutakuwa na ada katika kuweka pingamizi, bali pingamizi zizingatie matakwa ya ibara ya 11(2) ya kanuni za uchaguzi", alisema Ndolanga
Ratiba inaonesha Septemba 26 ni fursa ya kukata rufaa iwapo maamuzi yaliyotolewa na kamati DRFA hayakumridhisha mrufaa na hiyo itakwenda kwa kamati ya TFF na kampeni kwa wagombea zitaanza rasmi Oktoba 4, hadi 13 ambapo Oktoba 14 itakuwa uchaguzi.
Uchaguzi wa DRFA umejumuisha waandishi wa habari watatu waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali ambao ni Benny Kisaka, Shafii Dauda na Salum Mkemi ambaye jina lake limeenguliwa ila anayo nafasi ya kukata rufaa.
No comments:
Post a Comment