Pages

Monday, September 17, 2012

AFRICAN LYON :KILA ATAKAYKANYAGA UWANJA WETU NI KIPIGO TU SASA

Kikosi cha African Lyon
KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa African Lyon kutoka Nigeria Obina Salamusasa amesema mchezo ujao dhidi ya Polisi Moro watahakikisha wanafanya vizuri.

Obina aliliambia HABARI ZA MICHEZO kuwa watahakikisha wanaondoka na pointi tatu kwenye mchezo huo ambao utachezwa Chamazi siku ya Jumatano ambao  African Lyon ndio wenyeji

Kiungo huyo alisema sababu ya kufungwa na Simba ni baada ya wao kukosa penalti iliyopanguliwa na Juma Kaseja na Mrisho Ngassa kukimbia na Mpira kabla hajatoa pasi kwa Nassor Masoud "Cholo" aliyefunga bao la pili.

Pia alidai mwamuzi aliwabeba Simba kwa kutoa penalti ambayo anadai hawakustahili japo walifungwa walicheza vizuri sana na kocha ameshaanza kufanyia marekebisho makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wao na Simba.

"Unajua sisi hatutadharau timu yoyote kwani mchezo wa miguu ili ushinde unatakiwa kucheza kwa bidii na ligi ya mwaka huu kila timu inacheza kwa malengo ya kushinda tu", alisema Obina kwa kiswahili cha kuchanganya na kiingereza.

African Lyon ambayo uwanja wake wa nyumbani ni Chamazi wanadai watahakikisha kila timu inayotia mguu Chamazi inafungwa ili kujiweka katika nafasi nzuri mapema kwenye msimamo wa ligi.

African Lyon kwenye mchezo wa ufunguzi walifungwa na Simba bao 3-0 kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment