Pages

Friday, September 14, 2012

BFT YATEUA WAAMUZI UBINGWA WA TAIFA 2012

SHIRIKISHO la ngumi Tanzania (BFT) kwa kupitia chama cha  waamuzi wa ngumi za ridhaa wameteua waamuzi watakao tumika kuchezesha mashindano ya ubingwa wa taifa 2012.

Mashindano haya yanatarajiwa kufayika kuanzia Septemba 17-22 mwaka huu uwanja wa taifa wa ndani jijini Dar es salaam.

Akizungumza na HABARI ZA MICHEZO, Katibu Mkuu wa BFT Makore Mashaga alisema, Waamuzi walioteuliwa ni Mohamed Kasilamatwi ambaye ni mwamuzi wa kimataifa na Juma Selemani anayetambulika mwamuzi wa Afrika ambao watakuwa wasimamizi wa waamuzi.

Waamuzi wa ngazi ya taifa walioteuliwa ni Maneno Omari, Ridhaa Kimweli, Mohamed Bamtulla, Shija Masanja, Mafuru mafuru, Moshi makali, Hamza abdallah  na Marko Mwankenja.

Pia alisema mashindano ya Taifa yatashirikisha mikoa yote ya Tanzania na kuwataka kuendelea na mazoezi ili kuleta ushindani wa kweli.

"Mikoa ijiandae vizuri maana mashindano ya mwaka huu yatakuwa na ushindani sana",alisema Makore.

No comments:

Post a Comment