Pages

Friday, September 28, 2012

AZAM YASHIKILIA USUKANII WA LIGI KUU

Azam FC leo wameichezesha kwata timu ya JKT Ruvu ya Pwani bao 3-0 kwenye mchezo wa ligi ulochezwa uwanja wa Taifa.

Azam walipata bao la kuongoza katika kipindi cha Kwanza dakika ya 44 kupitia kwa John Bocco 'Adebayor' akifunga bao lake la kwanza msimu huu wa 2012/13 kwa mkwaju wa penati.


Kikosi cha JKT RUVU



Azam FC walirejea kipindi cha pili na kutawala mchezo na kufanikiwa kupata mabao mengine mawili kupitia kwa mapacha Kipre Herman Tchetche dakika ya 65 na Kipre Michael Balou dakika ya 79.

Mabao hayo yote yalitokea upande wa kulia wa timu JKT Ruvu ambao walionekana kuzidiwa kipindi chote cha mchezo 
Kwa hakika hata kama Azam wameshinda lakini hawakuonesha mchezo wenye ushindani na kwa upande wa JKT Ruvu midfield na straikers wanaonekana hawapo makini kabisa kwani bao walizofungwa mashambulizi yalikuwa yanaanzia nyuma na yalikuwa yanapita midfield kama hakuna mkabaji kati hivyo beki ilikuwa inalemewa.

 Azam FC wameiengua  kileleni mwa msimamo ligi Simba kwa muda hadi hapo kesho itakwaana na  Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye uwanja wa Taifa na mchezo huu utarushwa na kituo cha michezo cha Super sport kuanzia saa 11 jioni pia utakuwepo mchezo mwingine kwenye dimba la Sheikh Aman Karume jijini Arusha ambapo JKT Oljoro watawakaribisha wanajeshi wenzao wa JKT Mgambo ya Tanga.

No comments:

Post a Comment