Wachezaji wa copa coca cola wakiwa uwanja wa Karume kwenye mazoezi |
Wachezaji wa Copa coca cola wakimsikiliza kocha Kim Poulsen |
Timu hii ambayo inaundwa na wachezaji nyota 22 waliochaguliwa wakati wa mashindano ya Copa coca cola yaliyofanyika jijini na kushirikisha mikoa yote ya Tanzania ipo chini ya kocha Kim Poulsen na Silvester Marsh.
Akizungumza na HABARI ZA MICHEZO kocha msaidizi Silvester Marsh alisema timu ipo kambi kwa ajili ya maandalizi ya kwenda nchini Afrika ya kusini kufanya ziara ya mafunzo na kucheza mechi.
Safari ya timu hii inagharimiwa na coca coca ambayo ndio walikuwa wafadhili wa mashindano ya copa coca cola.
Marsh pia alitoa rai kwa mikoa kuendeleza wachezaji walioshiriki mashindano ya copa coca cola ili taifa liwe na timu bora za kila umri.
Pia aliipongeza Simba kwa kuwa program za vijana na akavita vilabu vingine viige mfano wa Simba, Azam, JKT Ruvu, Makongo na Baden Paul maana ndizo zenye timu za vijana zilizo bora.
No comments:
Post a Comment