Pages

Thursday, August 23, 2012

LIGI YAFIKA TAMATI DAR


UONGOZI wa chama cha soka la wanawake Dar es salaam (DWFA) umesema kuwa ligi msimu wa 2011/2012 itafikia kikomo leo kwenye uwanja wa Karume.

Akizungumza na habari za michezo katibu wa DWFA Stephania Kabumba alisema ligi itafika kikomo leo kwa timu za Mburahati kucheza na Sayari saa kumi jioni.

Pia alisema kuwa anategemea mchezo huo kuwa wa ushindani sana kwani timu hizo ni wapinzani wa jadi na Mburahati ndie anashikilia ubingwa baada ya msimu uliopita kuuchukua kutoka na tofauti ya mabao ya kufungwa na kufunga baada ya kulingana pointi na Sayari.

Mburahati ambayo inawashambuliaji wenye uchu wa kuzifumania nyavu wana nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa huo kwani ndio wanaoongoza ligi wakiwa na pointi 28  akifuatiwa na Sayari mwenye pointi 24 lakini sayari ana mchezo wa kiporo na Uzuri ambao wanasema wataupangia tarehe baada ya ratiba kukamilika.

Nafasi ya tatu inashikiwa na Tanzanite  ambayo ina pointi 19 na amemaliza michezo yake, nafasi ya nne ipo kwa Uzuri mwenye pointi 17 lakini amebakiza mchezo mmoja.

Simba queens pointi 12, Evergreen pointi 11 na Temeke queens anashikilia mkia akiwa hana pointi.

Ligi ya wanawake mkoa wa Dar es salaam imekosa msisimko kutokana na idadi ya timu kupungua kila msimu ambapo misimu miwili timu za JKT Queens na  Mndela hazijashiriki na msimu huu Emima haijashiriki.

Pia alisema tatizo linaloathiri timu ni kukosekana kwa wafadhili kitu ambacho timu zinalemewa na gharama za uendeshaji na kushindwa kumudu kujiendesha.
Mrisho Ngassa akifanya mazoezi gym jijini Arusha

Baadhi ya wachezaji wa Simba wakiwa gym kwenye kambi walioweka Arusha

Hapa tizi tu

Harun Moshi "Boban" akiwa gym na wenzake jijini Arusha

No comments:

Post a Comment