Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, February 11, 2018

SIMBA YAPIGA 4G KIMATAIFA LEO



SIMBA, leo imeendeleza msemo wake wa 4G mpaka kwenye michuano ya kimataifa baada ya kuifunga Gendarmerie mabao 4-0 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo ya michuano ya kombe la Shgirikisho Afrika, Simba ilifunga mabao matatu katika kipindi cha kwanza huku bao la nne ikilifunga dakika za mwisho za kipindi cha pili.
Wawakilishi hao kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho walianza kuhesabu mabao dakika ya kwanza ya mchezo huo baada ya Said Ndemla kufunga kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja kutikisa nyavu.
Nahodha wa Simba, John Bocco alifunga mabao mawili katika mechi hiyo, dakika ya 32 alilolifunga baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Gendarmerie na dakika ya 45 alipofunga bao la kichwa akiunganisha krosi ya Emmanuel Okwi.
Simba ilitawala katika kila idara kwenye kipindi cha kwanza, lakini hali ilibadilika kwenye kipindi cha pili baada ya wapinzani wao kuonekana kujizatiti zaidi.
Kujizatiti huko kwa Gendarmerie kuliwafanya Simba kupata tabu kuongeza mabao, hasa Okwi aliyeonekana kutatizika anapopiga mipira ya adhabu.
Pengine baada ya kujiuliza na kujirekebisha, dakika ya 90, Okwi aliandika bao la nne kwa Simba kwa mpira wa adhabu ulioanzishwa na Erasto Nyoni kabla ya ‘Mhenga’ huyo kuuwahi na kuujaza wavuni.
Shujaa mwingine katika mechi ya jana alikuwa kipa wa Simba, Aishi Manula aliyeoangua penalti katika dakika ya 50.
Penalti hiyo iliyopigwa na Abdorahim Mohammed ilitolewa na mwamuzi baada ya James Kotei wa Simba kumchezea rafu Ahamed Aden wa Gendarmerie.
Matokeo hayo yanaiweka Simba nafasi nzuri ya kusonga mbele kwani sasa wapinzani wake watalazimika kushinda 5-0 katika mechi ya marudiano ili wasonge mbele.
Akizungumza baada ya mechi hiyo, nahodha wa Simba, John Bocco alisema wamefurahia matokeo hayo na sasa wanaiandaa na mechi za Ligi Kuu kwani lengo lao ni kufanya vizuri.
Nahodha wa Gendarmerie alisema moja ya sababu za wao kupoteza mechi hiyo ni hali ya hewa ya joto kali.
“Simba ni timu kubwa, tumefurahi tumepata uzoefu zaidi nasi tutajipanga kwa mechi ijayo, huwezi jua kwenye soka lolote linaweza kutokea,” alisema.


No comments:

Post a Comment