Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, September 15, 2017

KARIBU LIGI DARAJA LA KWANZA MSIMU WA 2017/18

Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inatarajiwa kuanza Jumamosi Septemba 16, 2017 katika viwanja vinne tofauti nchini kwa mujbu wa ratiba iliyotoka mwezi uliopita.
Kwa mujibu wa Ratiba ya FDL, katika Kundi A: Mgambo itacheza na JKT Ruvu katika Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga wakati Kundi B: kutakuwa na michezo miwili.

Michezo hiyo miwili itakuwa ni kati ya Mawenzi Market itakayokuwa mwenyeji wa KMC ya Kinondoni, kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro wakati Mufindi United itakuwa mgeni wa Polisi Dar kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, Dar es Salaam.

Kundi C: kutakuwa na mchezo mmoja kwa siku ya Jumamosi ambako Rhino ya Tabora itakuwa mwenyeji wa Alliance Schools kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.

Ni ligi ya mabadiliko: Ligi ya msimu huu ina mabadiliko makubwa mawili yaliyopitishwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Kwanza ni kupandisha idadi ya timu zitakazopanda daraja badala ya tatu (moja kutoka katika kila kundi) hadi timu sita (timu mbili kutoka katika kila kundi) zitakazocheza Ligi Kuu msimu ujao wa 2018/19.

Ligi Kuu msimu ujao itakuwa na timu 20 kutoka timu 16 zinazoshiriki kwa sasa.

Kwa mujibu wa mabadiliko hayo, VPL msimu huu itashusha timu mbili tu na kubaki 14 ambazo zitasubiri sita zitakazopanda daraja.

Mabadiliko mengine yanahusu Kanuni ya 25 ambako sasa mara baada ya makato ya msingi katika mapato ya mlangoni, asilimia 60 itakwenda kwa timu mwenyeji badala ya kugawanywa kama ilivyokuwa awali.

Hii italeta juhudi kwa timu mwenyeji kuitangaza timu yake na mchezo wake kwa wadau wengi ili ivue mapato makubwa tofauti na miaka iliyopita ambako TFF imeona kwamba kulikuwa na kutegeana kutangaza mechi.

Makundi ya Daraja, kundi ‘A’ lina timu za African Lyon, Ashanti United, Friends Rangers na Mshikamano za Dar es Salaam wakati nyingine ni JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga na Mvuvumwa ya Kigoma.

Kundi ‘B’ ziko za Coastal Union ya Tanga; JKT Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mawezi Market NA Polisi Tanzania za Morogoro, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa na Polisi Dar Ya Dar es Salaam.

Kundi ‘C’ lina timu za Alliance School, Pamba na Toto

African za Mwanza, Rhino Rangers ya  Tabora, Bishara Mara ya Mara, Dodoma FC ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.

No comments:

Post a Comment