KAGERA Sugar
imecheza mechi tatu bila kupata ushindi
tangu kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya juzi kupokea
kipigi cha bao 1-0 toka kwa Azam FC uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex,
Dar es Salaam.
Katika
mchezo wa ufunguzi uliochezwa uwanja wa Kaitaba, Agosti 26, Kagera Sugar walifungwa
na Mbao FC 1-0 na mchezo uliofuata wakatoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Ruvu
Shooting.
Kocha wa
timu hiyo Mecky Maxime alisema bado ana matumaini ya kufanya vizuri na yupo
kwenye mbio za kuwania ubingwa kwani hajakata tamaa kwani
timu yake ilicheza vizuri kuliko wapinzani wao Azam FC
“Tumepoteza mchezo
wetu lakini nawapongeza wachezaji licha ya kufungwa bado waliendelea kucheza
vizuri. Hii ni ligi bado tuna nafasi ya kufanya vizuri na kushinda na hatimaye
kutwaa ubingwa.”
“Msimu
uliooita tulianza kwa kufanya vibaya karibu mechi nne za kwanza lakini msimu
huu hatutaki iwe hivyo. Nawaamini wachezaji watafanya vizuri, matokeo mabaya
waniachie mimi wao waendelee kucheza uwanjani,” alisema Maxime
Pia Maxime alisema wanahukumiwa kwa matokeo pekee lakini
walicheza vizuri muda mrefu, kosa moja wapinzani wakalitumia, wakafunga,
wanajipanga kwa mechi zijazo ili wafanye vizuri.
Naye kocha msaidizi wa Azam, Idd Cheche alisema ushindi
waliopata ulikuwa mgumu kwani Kagera walicheza vizuri ila wao walitumia nafasi
moja waliyoipata kujihakikishia ushindi.
“Haikuwa mechi rahisi, wapinzani walifanya vizuri tumepata
nafasi moja tumeitumia kupata pointi tatu nyumbani ni jambo la kumshukuru
Mungu,” alisema Cheche.
Kwa ushindi huo Azam imefikisha pointi saba baada ya kucheza
mechi tatu na kufunga mabao mawili huku nyavu zao zikiwa hazijaguswa.
No comments:
Post a Comment