Tuzo hiyo ni ile ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika msimu wa 2016/17 ambayo imeenda kwa Mohamed Hussein maarufu kwa jina la Tshabalala au Zimbwe Jr.
Zimbwe ambaye kawaida amefanikiwa kubeba tuzo hiyo akiwazidi wenzake wanne aliokuwa nao hadi dakika za mwisho katika kuwania kipengele hicho.
Katika shughuli hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, Tuzo nyingine ilikuwa kama ifuatavyo:
Bao Bora la Msimu imeenda kwa Shiza Kichuya wa Simba aliloifunga dhidi ya Yanga katika mzunguko wa pili, Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi imeenda kwa Mbaraka Yusuph wa Kagera Sugar, Tuzo ya Kocha Bora Mackie Maxime wa Kagera Sugar, Tuzo yaw Heshima imetua mwa Kitwana Manara.
Tuzo ya Mchezaji Bora wa Kigeni imechukuliwa na Haruna Niyonzima wa Yanga, Tuzo ya Mfungaji Bora imegawiwa mara mbili ambapo imeenda kwa Simon Msuva wa Yanga na Abdullaman Mussa wa Ruvu Shooting.
Mwadui FC imechukua Tuzo ya Timu Yenye Nidhamu. Tuzo ya Kipa Bora kachukua Aishi Manila wa Azam FC, Tuzo ya Mwamuzi Bora kachukua Erry Sasii, Tuzo ya Ismail Alan (yule mchezaji wa timu ya mbao aliyefia uwanjani) imechukuliwa na Shabani Idd wa Azam FC
Msuva akikabidhiwa tuzo ya ufungaji bora
Baba yake Mohamed Hussein akimchukulia tuzo mwanae
No comments:
Post a Comment