Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 29, 2017

Simba Waacha Kilio Dodoma

SIMBA juzi ilitawazwa kuwa bingwa mpya wa Kombe la FA baada ya kuifunga Mbao FC mabao 2-1 katika mechi ya fainali iliyochezwa uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na kuacha vilio kwa wachezaji wa Mbao.
Baada ya mechi kumalizika wachezaji wa Mbao walijikuta wakiangua kilio kwani waliamini kwamba Simba haikuwa na uwezo wa kutwaa ubingwa huo kutokana na jinsi walivyokuwa wamewabana.
Hata baada ya kukabidhiwa medali za mshindi wa pili wachezaji wa kikosi hicho chenye masikani yake jijini Mwanza hawakuwa na furaha zaidi ya kujutia penati ambayo Simba walipata baada ya Asante Kwasi kuunawa mpira.

Penati hiyo ilipigwa na Shiza Kichuya na kuifanya Simba imalize mechi ikiwa inaongoza katika dakika 30 za nyongeza kufuatia kumaliza kwa sare tasa katika dakika 90 za mchezo huo.
Benedict Haule ambaye ni kipa wa timu hiyo alisema kuwa, “Hata kama wamepata ubingwa huo lakini bado sisi ni bora kama wao, tulistahili kushinda hii mechi ila mwamuzi ndiye aliyeharibu, nilikuwepo golini na nilikuwa nashuhudia kila kitu.
“Naamini tungepata nafasi ya kuwa mabingwa tungefanya vizuri kwani kikosi chetu kingeimarishwa zaidi, tulianza vibaya kwenye ligi kwasababu ya presha lakini baadaye tulizoea na ndiyo maana tuliweza kufanya vizuri hivyo hata mashindano ya kimataifa tuna uwezo mkubwa tu tofauti na watu wanavyotufikiria,” alisema Haule