Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, May 29, 2017

Arsenal Kama Simba

LONDON, Uingereza
ARSENAL kama Simba nao wametwaa kombe la FA nchini Uingereza kwa kuifunga Chelsea mabao 2-1 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Wembley.
Jioni ya leo Simba ya Dar es Salaam ilitwaa kombe la FA kwa kuifunga Mbao FC idadi kama hiyo ya mabao katika mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
Mabao ya Arsenal yalifungwa na Alexis Sanchez na Aaron Ramsey huku bao la Chelsea likifungwa na Diego Costa.

Mwamuzi Anthony Tylor alimtoa nje kwa kadi nyekundu Victor Moses wa Chelsea dakika ya 68 kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano kwa mchezo usio wa kiungwana.

Ushindi huo unaweza kurudisha amani ndani ya Washika bunduki hao kwani wamekuwa wakishinikiza kocha Arsene Wenger kuachia ngazi kutokana na matokeo mabovu ya katika mechi zao.

No comments:

Post a Comment