Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Tuesday, January 3, 2017

TFF YAACHANA NA MKWASA, YAINGIA KWA MAYANGA




SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limemteua Salum Mayanga kuwa kocha wa muda wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’.
Mayanga anachukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia tamati  mwezi Machi.
Miongoni mwa majukumu ya Mayanga yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.

Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).

TFF imemshukuru Kocha Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.

No comments:

Post a Comment