Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, October 22, 2016

YANGA YAIADHIBU KAGERA 6-2 NA KUPANDA NAFASI YA PILI YA MSIMAMO Image result for yanga images
MAKIPA wa Kagera Sugar Hussein Shariff 'Casillas'  na David Burhan wameipa zawadi ya Wikiendi timu ya Yanga kwa kuruhusu kufungwa mabao matatu kila mmoja katika mchezo uliomalizika kwa wenyeji hao kulala mabao 6-2 kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Mchezo huo umezalisha mabao nane ambapo Casillas alifungwa mabao matatu mepesi katika dakika 27 pekee alizokuwa langoni kabla ya Kocha Mecky Mexime kumtoa na kumuingiza  David Burhan ambaye nae alifungwa matatu.

Cassilas alishindwa kujiamini langoni ambapo alifanya makosa kadhaa katika dakika chache alizodumu uwanjani ambapo kama washambuliaji wa Yanga wangeongeza umakini kabla ya mlinda mlango huyo kufanyiwa mabadiliko basi wangeweza kufunga zaidi ya mabao hayo kipindi cha kwanza.

Washambuliaji Obrey Chirwa na Donald Ngoma walifunga mabao mawili kila mmoja huku Simon Msuva na Deus Kaseke wakifunga moja moja na kukamilisha karamu hiyo ya mabao.

Mbaraka Yusuph alikuwa wa kwanza kuwapatia wenyeji bao la uongozi dakika ya tatu kwa kupiga shuti kali lililomgonga beki Andrew Vicent 'Dante' na kumuacha mlinda mlango Deogratius Munishi 'Dida' asijue la kufanya kabla ya kuongeza la pili kipindi cha pili.

Matokeo ya mechi nyingine zilizochezwa Leo
African Lyon 2-0 Mbeya City
Majimaji 1-0 Ruvu Shooting
Ndanda FC 1-2 Mwadui
Mtibwa Sugar 3-3 Stand United