Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, October 12, 2016

TFF: HATUTAMBUI MABADILIKO YA YANGA




SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema haitambui mababiliko ya uendeshwaji wa Klabu ya Yanga; badala yake wameuandikia uongozi wa Yanga barua wakitaka nakala ya mkataba wa ukodishwaji wa klabu hiyo kwa miaka kumi kwa mwekezaji anayetambulishwa Yanga Yetu.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine alisema kwamba TFF imekuwa ikipokea barua kutoka kwa wadau mbalimbali wa Yanga wakihoji taratibu au hatua zinazoendelea katika mfumo wa umiliki na uendeshwaji wa timu hiyo.
Mbali ya hatua hiyo, Alhamisi iliyopita ya Oktoba 6, 2016 vyombo mbalimbali vya habari (si HabariLeo) vilikuwa na taarifa kuhusu muhtasari wa mkataba wa Yanga wa kukodishwa na kampuni ijulikanayo kama Yanga Yetu Limited.
“Simba na Yanga wamekuja na mabadiliko ya kutaka kubadili mfumo wa uendeshaji na tukaziandikia kutaka kukutana nazo kutaka kujua uhalisia na Simba walikubali, lakini Kaimu Katibu Mkuu aliwajibu na kuwataka wawasiliane na wajumbe wa Baraza la Udhamini ndiyo wenye majibu juu ya mchakato wa ukodishwaji,” alisema Mwesigwa.
“Baadaye tunasikia kwenye magazeti kuwa kuna kampuni moja ambayo wamesaini nayo mkataba... Ndipo tukashtuka hivyo tunataka kujua status (hadhi) ya mkataba. Je, huo mkataba una husu timu A tu na programu za vijana itakuweje ndio vitu tunataka kujua japo klabu hiyo imesajiliwa kikatiba,” alisema Mwesigwa.
Kadhalika, Mwesigwa amesema wanataka kuona kilichopo kwenye mkataba kabla ya kushauri ili kuangalia kama vinakwenda sambamba na matakwa ya TFF, CAF na FIFA ili kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa yakiendelea kwani wengine wamefika hatua ya kuomba idhini ya TFF kwenda kumwona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli.
Mwesigwa alisema wanataka kujua pia nani anamiliki na nani anaendesha timu na umiliki wake ukoje kwa maana hizi timu za Simba na Yanga zinagusa nyoyo za watu wengi na taratubu za uhamishaji umiliki wake ukawa wa wazi-hadharani.
“Mambo ya kubadilisha uendeshwaji unatakiwa kufuata taratibu ikiwa ni pamoja kuenenda sawa na katiba ya klabu, kamati ya utendaji ifahamu, mkutano mkuu uridhie ili kujua nini kinauzwa na nini kinakodishwa ikiwa ni kwenye level (hatua) ya klabu.
“Kama itakuwa nje ya utaratibu wetu wa uendeshaji wa klabu kamati ya sheria na kamati ya utendaji watafanya kazi na kama watakuwa wamefuata taratibu inaweza isifike huko kwenye CAF na FIFA,” alisisitiza Mwesigwa.
Mwesigwa alisema TFF itaendelea kuwasiliana na Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit au Mwenyekiti, Yussuf Manji kwa mambo yote yanayohusu sera na mipango na siyo Bodi ya Wadhamini kama ambavyo Baraka alielekeza.
Pia Mwesigwa amesema hawaangalii tu mtu anayekodisha ana pesa kiasi gani bali hata kamapuni hiyo inatoka nchi gani na mmiliki ana historia gani huku amkimtolea mfano Roman Abromovich alipokwenda kununua Chelsea.
“Msimamo wa TFF  ni kwamba klabu ya Yanga ipo kama ilivyokuwa kwa mujibu wa taratibu za TFF, CAF na FIFA hadi hapo watakapo pata barua toka Yanga na wanatambua uongozi wa Mwenyekiti Yussuf Manji na Kaimu katibu Mkuu Deusdedit Baraka.

No comments:

Post a Comment