Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, October 15, 2016

SIMBA YAIFUNGA KAGERA SUGAR 2-0 UWANJA WA UHURU


VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wamezidi kujikita kileleni mwa msimamo baada ya kuichapa Kagera Sugar mabao 2-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Simba imepata ushindi katika mechi ya saba kati ya tisa ilizocheza na sasa imefikisha pointi 23 kileleni.
Wafungaji wa mabao ya Simba ni Mzamiru Yassin na Shizza Kichuya aliyefunga bao lake la saba.
Iliilazimu Simba kusubiri mpaka dakika 43 kuandika bao la kuongoza lililofungwa na Yassin baada ya kuunganisha mpira wa kona wa Kichuya.
Katika kipindi hicho, Simba ilionekana kutawala zaidi mechi hiyo huku wachezaji wake wakikosa mabao kadhaa.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na timu zikishambuliana kwa zamu lakini ni Simba ndiyo ilifaidika na mashambulizi hayo kwani iliandika bao la pili katika dakika ya 75.
Kichuja ndiye aliyefunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti iliyotolewa na mwamuzi Hussein Athumani wa Katavi baada ya Juma Ramadhani wa Kagera kumkwatua Mohamed Ibrahim kwenye eneo la hatari.
Katika mechi nyingine zilizochezwa jana, Stand United iliyokuwa nyumbani kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga ilipunguzwa kasi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 ma African Lyon.
Stand sasa inaendelea kushika nafasi ya pili ikiwa na pointi 21 huku Lyon ikifikisha pointi 10 katika nafasi ya 11 kwenye msimamo huo wa ligi inayoshirikisha timu 16.
Kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi, JKT Ruvu imelazimishwa sare ya bao 1-1 na Mwadui na kuifanya iendelee kushika nafasi ya 14 ikiwa na pointi nane.
Mwisho.