Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, October 8, 2016

LIGI KUU KUENDELEA LEO PAMOJA NA LIGI DARAJA LA KWANZA

Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea leo kwa michezo mitatu ambako Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Wakati African Lyon itaikaribisha Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam JKT Ruvu yenyewe itaialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi ulioko mkoani Pwani.
Kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza, kundi A kutakuwa na mchezo kati ya Pamba ya Mwanza na Polisi Dar kwenye CCM Kirumba wakati African Sports itakuwa mwenyeji wa Kiluvya United kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Ligi hiyo ya Daraja la Kwanza itaendelea Jumapili Oktoba 9, 2016 kwa mchezo utakaozikutanisha Ashanti United na Friends Rangers; zote za Dar es Salaam. Kadhalika Jumatatu, kutakuwa na mchezo kati ya Mshikamano ya Dar es Salaam na Lipuli ya Iringa. Mchezo huo, pia utafanyika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Kundi B leo kutakuwa na mchezo kati ya Kurugenzi ya Iringa na Coastal Union ya Tanga ufakaofanyika huko Mufindi ukifuatiwa na michezo mitatu siku ya Jumapili Oktoba 9 ambayo Mlale itacheza na Polisi Moro huko Uwanja wa Majimaji, mjini Songea wakati Njombe Mji itaikaribisha Kemondo wakati KMC itacheza na Mbeya Warriors kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani.
Kundi C leo Mvuvumwa ya Kigoma itacheza na Singida United ya Singida wakati Panoni itapambana na Alliance huku Polisi Dodoma itacheza na Polisi Mara wakati Jumapili Rhino ya Tabora itakuwa mwenyeji wa Mgambo JKT ya Tanga.

No comments:

Post a Comment